Moroto aitaka wizara ya elimu kuwa na Subira
Huku Walimu Wakitarajiwa Kuwasili Kwenye Shule Tofauti Tofauti Nchini Kufuatia Agizo La Wizara Ya Elimu Ili Kuzikagua Hali Kabla Ya Wizara Hiyo Kutangaza Siku Ya Wanafunzi Kurejelea Masomo Yao, Mbunge Wa Kapenguria Samuel Moroto Ameitaka Wizara Ya Elimu Kuchukua Muda Kabla Ya Agizo La Kurejelewa Kwa Masomo Shuleni.
Kulingana Na Moroto, Shule Nyingi Hazijaweka Mikakati Kabambe Ya Kuwatunza Wanafunzi Shuleni Dhidi Ya Maambukizi Ya Virusi Vya Korona.
Moroto Aidha Amepinga Pendekezo La Wizara Ya Elimu Ya Kuharakisha Kufanyika Kwa Mtihani Wa Kitaifa Huku Akidai Kwamba Wanafunzi Wengi Hawakuwa Na Uwezo Wa Kufuatilia Masomo Mtandaoni Kama Ilivyoagizwa Na Wizara Ya Elimu.
Wakati Huo Huo Moroto Ameisifia Hali Ya Amani Ambayo Imerejelewa Katika Eneo La Turkwel Mpakani Pa Kaunti Ya Pokot Magharibi Na Ya Turkana.
Hata Hivyo Ametaka Wizara Ya Elimu Kutumia Fursa Hiyo Ya Utulivu Kuzifufua Shule Ambazo Zilikuwa Zimesambaratika Kutokana Na Vita Na Wizi Wa Mifugo Baina Ya Jamii Ya Turkana Na Jamii Ya Pokot.