Mwanamme Wa Miaka Ishirini Na Tisa Awalawiti Vijana Wawili Wa Miaka Minane Na Saba Mtawalia Katika Mtaa Wa Shikangania, Kakamega

Maafisa Wa Polisi Wanamzuia Mwanamme Wa Miaka Ishirini Na Tisa Kwa Tuhuma Za Kuwalawiti Vijana Wawili Wa Miaka Minane Na Saba Katika Mtaa Wa Shikangania Viungani Mwa Mji Huo.

Kulingana Na Mamake Mmoja Wa Wathiriwa Lucy Inyanji Ni Kwamba Mwanawe Amekuwa Akipitia Hali Ngumu Kila Anapokwenda Haja Baada Ya Kutendewa Unyama Huo.

Naye Mamake Mshukiwa Sarah Were Amekiri Kwamba Mwanawe Amekuwa Kero Katika Jamii Kwa Kutekeleza Maovu Mara Kwa Mara.