BABA AMBAKA MWANAWE WA KIKE MWENYE UMRI WA MIAKA 14

BARINGO

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Baringo wameanzisha uchunguzi wa kumsaka baba ambaye anadaiwa kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 14 na kumtunga mimba kabla ya kumshurutisha kuavya mimba hiyo wikendi iliyopita.

Kulingana na msichana huyo ambayo ni mwanafunzi wa darasa la saba ni kwamba babake amekuwa akimtendea unyama huo tangu alipokua mchanga nyumbani kwao katika eneo la Kabartonjo eneo la Baringo Kaskazini.

Msichana huyo amedai kuwa babake alimshurutisha kumeza dawa za kuavya mimba huku akimtaka kutofichua kwa yeyote kuhusiana na hilo.

Kisa hicho kimeripotiwa katika kituo cha polisi cha Kabarnet.