WAZIRI MAGOHA ATARAJIWA KUZURU KATIKA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

Waziri Wa Elimu Prof George Magoha Anatarajiwa Kuzuru Kaunti Hii Ya Pokot Magharibi hii leo Ili Kutathmini Tenda Ya Madawati Iwapo Imekamilika.

Magoha Anatarajiwa Kuzuru Shule Ya Upili Ya Tomena Na Baadae Kuelekea Shule Ya Msingi Ya Psigirio Na Kumalizia Ziara Yake Katika Shule Ya Upili Ya Mnagei.

Wakati Uo Huo Magoha Anatarajiwa Kuangazia Maswala Ya Virusi Vya Corona Iwapo Shule Hizo Zinaweza Kuwashughulika Wanafunzi Shule Zinapotarajiwa Kufunguliwa Mwaka Ujao.

Ikumbukwe Magoha Amekuwa Akifanya Misusururu Ya Kuzuru Shule Mbali Mbali Ili Kuangazia Utayarifu Wa Shule Hiyo.

Ikumbukwe Hivi Maajuzi Magoha Alipozuru Shule Ya Msingi Ya Lagas Kwenye Kaunti Ya uasingishu alionekana Akimdhalalisha Mkurugenzi Wa Elimu Kwenye Kaunti Hiyo Gitonga Mbaka Kwa madai Kuwa Amefeli Kwenye Majukumu Yake.

Hata Hivyo Shinikizo Zimekuwa Zikitolewa Kuwa Magoha Amuombe Msamaha Mbaka Lakini Magoha Kamwe Amesema Kuwa Hatafanya Hivyo.