ZOEZI LA KUWATEUWA MAKURUTU WA KDF LAENDELEA KWA SIKU YA PILI KATIKA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Zoezi la kuwaajiri vijana katika Idara ya ulinzi nchini KDF imeendelea kwa siku ya pili hii leo katika kaunti hii ya Pokot Magharibi katika eneo la Chepareria.
Hiyo jana zoezi hilo lilifanyika katika uwanja wa Makutano ambapo vijana zaidi ya mia moja walijitokeza kwa minajili ya zoezi hilo.
Akizungumza na wanahabari baada ya kukamilika kwa zoezi hilo , mmoja wa maafisa waliosimamia shughuli hiyo nzima Leftanand Kano Gichuhi amesema waliweza kuwasajili makurutu kumi na watatu ambapo wanaumme walikuwa kumi na wawili na msichana mmoja.
Hata hivyo kamati ambayo iliendesha zoezi hilo imetilia maanani mahitaji yote yanayohitajika katika uajiri huo.
Kuhusiana na suala la ufisadi kwenye ajira zote nchini Gichuhi amewataka vijana wote nchini kushirikiana katika kuukomesha ufisadi huo kwa kukataa kupeana hongo huku akidai kwamba vijana wengi wangali wanaamini kwamba ajira hutokana na hongo, hali ambayo amesema inahatarisha utendakazi katika nyanja zote za ajira nchini.