ZOEZI LA KUTWAA SILAHA KWA LAZIMA KUANZA KUTEKELEZWA RASMI MWISHONI MWA MWEZI HUU


Mshirikisha wa usalama kanda ya Rift Valley George Natembeya amesema kuwa zoezi la kutwaa kwa lazima silaha zinazomilikiwa kwa lazima kinyume na sheria kwenye eneo hilo litaanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza na wanahabari Nataembeya amesema kuwa mda wa kuzisalimisha silaha hizo kwa hiari ulikamilika bila mafanikio.
Natembeya amesema kuwa shughuli hiyo ilijikokota kutokana na kuzuka kwa janga la korona nchini.
Matamshi ya Natembeya yanajiri siku mbili tu baada ya mtu mmoja kuawa na mwingine kujeruhiwa kule Kapedo kwenye jaribio la wizi wa mifugo.
Kaunti za Baringo na Turkana ndizo kaunti ambazo zinalengwa zaidi.