‘ZIARA YA RAIS RIFT VALLEY ITAKUWA NA UFANISI MKUBWA’ ASEMA MOROTO.


Tofauti baina rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto hazitaathiri kwa vyovyote ziara ya rais inayopangiwa eneo la rift valley ambalo ni ngome yake Ruto.
Haya ni kwa mujibu wa mbunge wa Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto ambaye amesema kuwa ziara ya rais si ya kibinafsi bali ni ya kutekeleza maendeleo kwa ajili ya wananchi.
Moroto amesema kuwa Ruto pamoja na wandani wake eneo la rift valley wataandamana na rais katika ziara hiyo.
Kauli yake Moroto inajiri wakati ambapo kumekuwepo na wasiwasi kuwa huenda rais akakosa mapokezi yanayohitajika kutoka kwa wendani wa Ruto, kufuatia tofauti ambazo zimekuwa zikishuhudiwa baina ya wawili hao tangia walipoingia afisini kwa muhula wao wa pili.