ZIARA YA RAIS MAGHARIBI YA NCHI YAIBUA MATARAJIO MAKUU
Wakazi wa kaunti ya Trans nzoia wameelezea matumaini kuwa rais Uhuru Kenyatta atatenga muda wa kuzuru kaunti hiyo hata baada ya kuahirishwa ziara yake eneo la magharibi.
Kulingana na mwenyekiti wa kiboroa squatters Alliance Inea Masinde, ziara ya rais itatoa suluhu kwa baadhi ya miradi iliyokwama kaunti hiyo mbali na mustakabali wa kisiasa eneo zima la magharibi ya nchi kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Aidha Masinde ameelezea kukerwa na mwendo wa pole wa ujenzi wa barabara ya Kitale-Endebes hadi Swam wa kima cha shilingi bilioni 4.5 na ule wa Lesos-Namanjalala-Kolongolo-Chepchoina wa kima cha shilingi bilioni 2.3.