ZAIDI YA WATU ALFU 3 WACHANJWA DHIDI YA CORONA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Jumla ya watu alfu 3,269 wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya corona kufikia sasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Haya ni kwa mujibu wa waziri wa afya katika kaunti hii Christine Apakoreng ambaye amesema kuwa chanjo hiyo bado ipo kwa wingi huku akiwahimiza wakazi walio katika kundi la awamu ya kwanza ya kupokea chanjo hiyo kujitokeza kwa wingi na kuipokea.
Aidha Apakoreng amesema serikali ya kaunti hii imeendelea kuweka mikakati zaidi ya kuhakikisha msambao wa virusi hivi miongoni mwa wakazi unadhibitiwa akiwahimiza wakazi kuendelea kuzingatia masharti yaliyowekwa.
Kando na hayo Apakoreng amesema serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha dawa za kutosha katika vituo vya afya kaunti hii.