ZAIDI YA WATU ALFU 14,000 WACHANJWA DHIDI YA CORONA TRANS NZOIA.

Na Benson Aswani
Waziri wa afya Kaunti ya Trans Nzoia Clare Wanyama amepongeza hatua zilizopigwa na wahudumu wa afya katika kukabiliana na janga la Covid19 nchini.
Akihutubu baada ya kuzuru kituo cha kutoa chanjo ya Covid 19 eneo la Kipkeikei eneo bunge la Cherangani Wanyama amesema wizara yake imetenga zaidi ya vituo 36 vya utoaji wa chanjo hiyo, huku zaidi ya watu 14,000 wakiwa wapokea chanjo hadi kufikia sasa.
Aidha Wanyama ametoa wito kwa umma kutokubali kupotoshwa kuhusu chanjo hizo akisema chanjo hizo zote zimethibitishwa na kuidhinishwa na shirika la afya duniani WHO, akitoa wito kwa umma kukumbatia chanjo hiyo ili kuimaris kinga ya mwili dhidi ya virusi vya corona.
Kwa upande wake mshirikishi wa shirika la Cliton Health Asses Initiative (CHAI) Victoria Mbeki amesema shirika hilo linashirkiana na serikali ya Kaunti ya Trans-Nzoia kwa kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya na kupelekea kufikia wananchi wengi zaidi kupata chanjo dhidi ya covid 19.