ZAIDI YA WATAHINIWA MILIONI MOJA HAWAWEZI KUAFIKIA ASILIMIA 50 YA ALAMA STAHIKI KWENYE BAADHI YA MASOMO


Baraza la Mitihani nchini KNEC imesema kuwa zaidi ya watahiniwa milioni 1 wa KCPE mwaka huu hawawezi kuafikia asilimia 50 ya alama stahiki katika masomo mbali mbali.
Baraza hilo liliandaa ripoti hiyo ili kutathmini uwezo wa wanafunzi baada ya janga la korona unaashiria kwamba wanafunzi wengi walifeli kwenye masomo ya Kiswahili, Kiingereza na ile ya ishara.
Mtihani wa kitaifa wa KCPE unatarajiwa kufanyika kati ya machi tarehe 22 na 24 mwezi huo.