WIZI WA PIKIPIKI WARIPOTIWA MJINI MAKUTANO KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Wahudumu wa boda boda katika kaunti hii ya Pokot Magharibi wameendelea kulalamikia wizi wa pikipiki ambao umeonekana kukithiri hasa mjini makutano.
Wahudumu hao sasa wanadai wezi hao wamebadili mbinu ambapo wanabadilisha rangi ya pikipiki zilizoibwa.
Hata hivyo wamesema kuwa kwa sasa wamenasa pikipiki mbili ambazo tayari zilibadilishwa rangi.
Wametoa wito kwa wahudumu wote kuwa makini kwani visa hivi vimeonekana kuongezeka zaidi katika siku za hivi karibuni.