WIZI WA PIKIPIKI WAKITHIRI POKOT MAGHARIBI
Wahudumu boda boda katika kaunti hii ya pokot magharibi wameendelea kulalamikia ongezeko la wizi wa pikipiki.
Kilio cha wanaboda boda hao kinajiri baada ya pikipiki moja kuibiwa eneo la Maili 11 siku ya jumamosi usiku na kudaiwa kuelekezwa eneo la Talau.
Wahudumu hao wamesema kuwa wengi wao wameibiwa pikipiki hizo licha ya kuwa zimechukuliwa kwa mikopo.
Wahudumu hao wametoa wito kwa idara za usalama kaunti hii ya Pokot Magharibi na serikali kuu kuingilia kati na kuwahakikishia usalama wanapotekeleza majukumu yao ya kujitafutia riziki ya kila siku.