WIZI WA MITAMBO YA SOLA SHULENI KACHELIBA VYAKITHIRI.


Visa vya wizi wa mitambo ya sola shuleni vimeripotiwa kukithiri eneo la Kacheliba katika kaunti hii ya Pokot magharibi shule ya wasichana ya St Bakhita ikiathirika pakubwa na wizi huo.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Kakuko mitambo hiyo imeibwa kwa mara ya pili sasa katika shule hiyo, kisa cha kwanza kikitekelezwa mwaka jana huku mtambo wa pili ukiibwa mapema juma hili, hali anayosema inawapelekea wakati mgumu kuwashughulikia wanafunzi shuleni humo.
Ametoa wito kwa viongozi na jamii ya eneo hilo kushirikiana na shule hiyo katika kuhakikisha kuwa mtambo huo unapatikana kwani kulingana naye huenda ni mtu wa karibu eneo hilo aliyeiba mtambo wenyewe kutokana na jinsi alivyoundoa.
Ni wito ambao umekaririwa na mwenyekiti wa kamati ya miundo msingi katika shule hiyo Renson Apakamoi ambaye aidha ametahadharisha umma dhidi ya kununua mtambo huo na badala yake kutoa ripoti kwani huenda ukasababisha maafa kutokana na viwango vya moto unaotoa.

[wp_radio_player]