WIZI WA MIFUGO WATEKELEZWA TIRIOKO BARINGO KAUNTI


Idadi ya Mifugo isiyojulikana imeibwa katika eneo la Kerio kwenye Wadi ya Tirioko kaunty ya Baringo, wizi ambao umetekelezwa na Watu wanaoaminika kutoka katika jamii ya Marakwet japo hakuna Mauaji ambayo yameripotiwa.
Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, Mwakilishi wadi Ya Tirioko Sam Lokales amesema Mifugo hao wanadaiwa kufichwa katika eneo la Naitirir kwenye kaunti ya Elgeiyo Marakwet.
Hata hivyo Lokales ametoa wito kwa Watu wa Jamii ya Pokot kukoma kulipiza kisasi katika tukio hilo badala yake wasubiri hatua za Serikali za kuwachunguza wezi hao hadi watakaporejesha Mifugo hao.
Kisa hicho kimejiri wiki chache tu baada ya Wanafunzi wawili katika eneo la Chesegon kupigwa Risasi na kujeruhiwa vibaya na watu wanaoaminika kutoka jamii iyo hiyo ya Marakwet.