WIZI WA MIFUGO WAREJELEWA ENO LA KARITA BAADA YA KUPINGWA MWAFAKA WA NABILATUK

Visa vya uvamizi na wizi wa mifugo baina ya jamii za Pokot na Karamoja eneo la Karita mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na taifa jirani la Uganda vimeanza kuhuhudiwa tena hali inayodaiwa kuchochewa na kupingwa mwafaka wa nabilatuk na bunge la uganda.

Hii ni baada ya wavamizi kutoka jamii ya Karamoja kudaiwa kutoweka na takriban ng’ombe 22 eneo la Kamongoy siku tatu zilizopita ambapo hadi kufikia sasa juhudi za kuwarejesha hazijafua dafu.

Wakazi wa eneo hilo sasa wanamlaumu rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kile wanachodai anaegemea jamii moja katika kutwaa silaha zinazomilikiwa na raia kinyume cha sheria wakitaka shughuli hiyo kutekelezwa kwa jamii zote.