WIZI WA MIFUGO BAINA YA JAMII ZA POKOT NA KARAMOJA WARIPOTIWA KUKITHIRI.

Visa vya utovu wa usalama baina ya jamii za Pokot na Karamoja mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na taifa jirani la Uganda vimeripotiwa kukithiri siku za hivi karibuni.
Kulingana na mbunge wa Kacheliba Mark Lumnokol, visa hivi vinasababishwa pakubwa na wizi wa mifugo baina ya jamii hizi mbili.
Hata hivyo Lumnokol amepongeza vikosi vya usalama vya upande wa Uganda ambavyo vimehakikisha kuwa mifugo ambayo inaibwa kutoka upande wa Kenya wanarejeshwa.
Aidha Lumnokol amesema kuwa serikali ya kaunti hii kwa ushirikiano na ile ya Uganda wanafuatilia kuhakikisha kuwa mifugo ambayo haijapatikana inapatikana akielezea imani ya kurejeshwa mifugo wote walioibwa.