WIZARA YA ELIMU KUANZISHA UJENZI WA MADARASA SITA KATIKA SHULE YA UPILI YA MNAGEI

POKOT MAGHARIBI


Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Upili Ya Mnagei Ann Lotuliatum Ameipongeza Wizara Ya Elimu Kwa Kuanzisha Ujenzi Wa Madarasa Sita Katika Shule Hiyo Hali Ambayo Inatarajiwa Kurahisisha Vita Dhidi Ya Maambukizi Ya Virusi Vya Korona Iwapo Wanafunzi Wote Watarejelea Masomo Yao Januari Mwaka Ujao Jinsi Wizara Ya Elimu Imetangaza.
Akizungumza Ofisini Mwake Baada Ya Waziri Wa Elimu Prof. George Magoha Kuzuru Shule Hiyo, Lotuliatum Aidha Amesema Watahiniwa Wanne Miongoni Mwa Mia Moja Ishirini Na Tisa Hawajukani Waliko Tangu Watahiniwa Wote Nchini Kuagizwa Kurejea Shuleni Kwa Matayarisho Ya Mitihani Itakayofanyika Mwaka Ujao.
Vile Vile Amesema Tayari Shule Yake Imepokea Madawati Hamsini Kutoka Kwa Wizara Ya Elimu.