WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUWACHAGUA VIJANA KWA WINGI TAREHE TISA MWEZI WA NANE KWA UONGOZI BORA


Ipo haja ya vijana nchini kuungwa mkono na watu wa matabaka yote nchini ili pia wadhihirishe uongozi wao hasa ikizingatiwa kwa kipindi kirefu uongozi wa taifa umekuwa mikononi mwa watu wenye umri wa juu zaidi huku vijana wakisalia kuahidiwa uongozi siku za usoni.
Swala la vijana na uongozi nchini limeendelea kuibua hisia kali miongoni mwa vijana kaunti hii ya pokot magharibi vijana wengi wakihisi kwamba ni vyema wakubaliwe kuwania wadhfa wowote humu inchini bila kuzuiliwa.
Henry sonko ambaye ni mwana boda boda katika kaunti ya pokot magharibi, amesema kuwa ni vyema vijana kuandaliwa mapema ili kuwa viongozi bora siku za usoni, akitolea mfano anavyohangaishwa mwaniaji kiti cha ubunge cha mathare kaunti ya Nairobi Bahati Kioko.
Vile vile Meshack lokorwa pia anasema kuwa vijana wengi wameachwa inje na badala yake wazee kukatalia viti, jambo ambalo linawakera wao kama vinjana, kwa sababu hiyo anatoa wito wake kwa serikali kuwa wao kama vijana watengewe asilimia 70 ya nafasi serikalini huku wazee wakitengewa asilimia 30 ya nafasi hizo.