WITO WATOLEWA KWA VIONGOZI KUWAFANYIA WANANCHI MAENDELEO KATIKA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI NA BENSON AWASNI


Aliyekuwa mwakilishi wadi mteule Lucy Lotee amemsuta vikali mwakilishi wadi ya kapenguria katika kaunti hii ya Pokot magharibi Emmanuel Madi kwa kile amedai kutowajibika katika majukumu yake.
Bi. Lotee ambaye ametangaza nia ya kugombea kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti amesema kuwa wakazi wa wadi ya Kapenguria wanakumbwa na changamoto nyingi kufikia huduma muhimu hali hamna hatua ambazo zinachukuliwa na mwakilishi wadi huyo kuangazia hali hii licha ya kuwa karibu na mwananchi.

Lotee amesema kuwa ni kutokana na hali ambapo ameamua kugombea kiti cha mwakilishi wadi ya Kapengurai ili kuhakikisha kuwa mwananchi ambaye ni mkazi wa wadi hii anapata huduma inavyostahili akiwahakikishia wakazi huduma bora iwapo atapewa nafasi hiyo.

Wakati uo huo Lotee amewataka wakazi wa eneo hili hasa vijana ambao hawajasajiliwa kuwa wapiga kura kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa wingi kusajiliwa ili kuwa katika nafasi bora ya kuwachagua viongozi wanaowapendelea.