WITO WA USALAMA WAENDELEA KUTOLEWA NA VIONGOZI WA BONDE LA KERIO.


Wito umetolewa kwa wakazi wa kaunti za bonde la Kerio kukumbatia amani na kutojihusisha na maswala ya uvamizi ambao umegharimu maisha ya wakazi wengi huku baadhi wakilazimika kuyakimbia makazi yao.
Ni wito wake mgombea kiti cha mbunge eneo bunge la Pokot kusini kaunti hii ya Pokot magharibi James Teko ambaye aidha amewataka wakazi wa kaunti za Pokot Magharibi Baringo, Elgeyo marakwet na turkana kushirikiana na kuwatambua wahalifu wanaoendeleza uovu huo ili wakabiliwe kisheria.
Aidha Teko amesema kuwa ni jukumu la kila kiongozi kutoka katika kaunti hizi kuhakikisha kuwa wakazi wanaishi kwa amani kwa kujizuia kutoa matamshi ambayo huenda yakachochea wakazi kutoka jamii moja kuinuka dhidi ya jamii nyingine.
Wakati uo huo teko ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanasiasa hasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi kuendesha kampeni za amani hasa wakati huu ambapo taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu wa terehe 9 mwezi agosti.