WITO WA MBUNGE WA MUMIAS MASHARIKI BENJAMIN WASHIALI

MUMIAS MASHARIKI


Huku idadi kubwa ya wakenya wakiwemo wahudumu wa afya wakiendelea kuripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa corona mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali amewataka wenyeji wa eneo hilo kufuata masharti ya wizara ya afya ilikuzuia msambao zaidi wa virusi vya corona.
Akiongea kwenye hafla ya mazishi,Washiali amewataka wenyeji kufuata masharati ya kukabili janga la corona kukiwemo kunawa mikono kila wakati bila kukoma pamoja na kuvalia barakoa kila wakati.
Kauli yake imetiliwa uzito na seneta mteule Naomi Shionga ambaye pia amewataka viongozi kujitokeza na kuwasaidia wenyeji wasiojiweza kupata vifaa vya kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.