WITO WA KUUNGANISHWA RAIS NA NAIBU WAKE WAENDELEA KUUNGWA MKONO.
Baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini wameendelea kuunga mkono pendekezo la baraza la maaskofu nchini kupewa fursa ya kuwaunganisha rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.
Akizungumza katika kanisa la mafuta pole eneo la kaptulwo kaunti hii ya pokot magharibi, mbunge wa Endebes kaunti ya trans nzoia Robert Pukose ambaye ni mwandani wa Ruto amesema kuwa hatua hiyo ni nzuri huku akikariri kauli ya Ruto kuwa yuko tayari kwa mazungumzo hayo.
Wakati uo huo Pukose amedai kuwa tofauti baina ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto zilisababishwa na mwafaka baina ya rais Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila odinga hatua ambayo ilipelekea wandani wa Ruto kufurushwa katika kamati mbali mbali bunge.