WITO WA AMANI WATOLEWA BAINA YA KAUNTI ZA POKOT MAGHARIBI NA ELGEYO MARAKWET.


Wito umetolewa kwa viongozi wa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet kuandaa mazungumzo ya kumaliza visa vya uvamizi ambao umegharimu maisha ya wakazi wengi.
Ni wito ambao umetolewa na mwakilishi wadi maalum eneo la Lomut Nancy Chombir kufuatia kisa cha mapema juma hili ambapo mkazi mmoja wa kaunti hii ya Pokot magharibi aliuliwa huku mwingine akijeruhiwa vibaya katika uvamizi uliotokea eneo la Chesogon.
Aidha Chombir amewataka wakazi kaunti hii hasa wanaoishi maeneo ambako kumekuwa kukishuhudiwa utovu wa usalama kuzingatia amani.