WITO WA AMANI WASISITIZWA TAIFA LINAPOELEKEA KWENYE UCHAGUZI MKUU.


Wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi wametakiwa kudumisha amani hasa wakati huu ambapo taifa linaeleka katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Ni wito wake Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye amehimiza utulivu ambao unashuhudiwa hasa maeneo ya mipakani pa kaunti hii na kaunti jirani hasa Turkana na trans nzoia akielezea imani ya hali hiyo pia kuafikiwa katika mpaka wa kaunti hii na kaunti ya Elgeyo marakwet.
Moroto amesema uchumi wa maeneo ya mipakani pa kaunti hii ya pokot magharibi umeathirika kwa kipindi kirefu kutokana na swala la utovu wa usalama na sasa ni wakati wakazi wa maeneo hayo wanastahili kutekeleza shughuli zao bila ya hofu ili kuimarika kiuchumi.