WITO UNAZIDI KUTOLEWA KWA SERKALI KUINGILIA KATI NA KUHAKIKISHA KWAMBA USALAMA UNADUMISHWA ENEO LA CHESOGON
Wakaazi eneo la lomut katika kaunti ya pokot magharibi wamekuwa wa hivi punde kujitokeza kushtumu visa vya utovu wa usalama mipakani pa kaunti hii ya pokot magharibi na elgeyo marakwet .
Wakiongozwa na francis chulianyang mkaazi wa wadi ya lomut wamesema hali hiyo imewapelekea kuishi kwa hofu ya usalama wao na mifugo yao.
Wakaazi hao sasa wanaitaka serikali kuwatuma maafisa zaidi wa usalama maeneo hayo ya mipakani ili kushika doria wakati kabla na baada ya uchanguzi.
Vile vile mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti hii ya pokot magharibi Simon kachapin amedai hali hii imechangiwa na baadhi ya wanasiasa wanaowachochea wakaazi wa maeneo haya akiahidi kuwa serikali yake itaakikisha suluhu inapatikana.