WITO UMETOLEWA KWA WANASIASA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KUTOINGIZA SIASA KATIKA MASUALA YA CHAKULA.


Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amemshutumu gavana johna lonyangapuo kwa kile amedai kutumia msaada wa chakula ambao unatolewa na serikali kwa kaunti zinazokabliwa na ukame kuendeleza ajenda zake za kisiasa.
Akipongeza hatua ya serikali kutoa chakula hicho kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi, seneta Poghisio amewataka wakazi wa kaunti hii kutohadaiwa na gavana lonyangapuo kuwa ni chama chake ndicho kimefanikisha kuletwa chakula hicho bali ni mpango wa serikali kwa kaunti 23 za maeneo kame nchini.
Poghisio ameisuta serikali ya gavana Lonyangapuo kwa kile amedai kuwa imeshindwa kuweka fedha za dharura kwenye bajeti yake ili kushughulikia majanga katika kaunti hii na sasa inatumia mipango ya serikali kuu kuendeleza sera zake.
Ppoghisio sasa anamtaka gavana Lonyangapuo kuzingatia uwazi katika ugavi wa chakula hicho ili kuhakikisha wakazi wote wanaolengwa katika pango huo wanapokezwa chakula hicho.