WEZI WA MIFUGO BONDE LA KERIO WAAHIDIWA MAKABILIANO MAKALI.


Mshirikishi wa usalama katika ukanda wa bonde la ufa mohammed maalim ametoa onyo kali kwa wahalifu wanaoendeleza uvamizi na wizi wa mifugo katika eneo la bonde la kerio.
Akiongea katika eneo la tot maalim amesema kuwa serikali itawakabili vilivyo wahalifu hao ili kurejesha utulivu katika eneo hilo ambalo limeshuhudia misururu ya mashambulizi siku za hivi karibuni.
Maalim amesema kuwa kwa sasa serikali inaendeleza mipango ya kuanzisha kambi ya maafisa wa gsu katika eneo la kapkobil kama moja ya mikakati ya kuwakabili wezi wa mifugo.
Maalim aidha amesema kuwa kambi ya maafisa wa kukabiliana na wizi wa mifugo (anti stock theft unit) itaanzishwa kwenye eneo la kolowa kwani ni ahadi iliyowekwa na serikali.
Wakati uo huo maalim amesisitiza kwamba kando na serikali kila mwananchi na pia kiongozi katika kaunti zinazoshuhudia utovu wa usalama ana jukumu la kutekeleza katika kurejea kwa usalama kwenye maeneo hayo.