‘WEZI WA MAJI’ WAKAMATWA TRANS NZOIA.
Washukiwa kumi na sita akiwemo mshukiwa mkuu anayeunganisha maji kinyume cha sheria katika kaunti ya transnzoia wamekamatwa ikisemekana kwamba ni mafundi wa kibinafsi wanaolaumiwa kutokana na ongezeko la visa vya wizi wa mita
Kwa mjibu wa meneja wa kampuni ya nzowasco kanda ya magharibi mark werunga wamekuwa wakipata hasara ya maelfu ya pesa kufuatia kuunganishwa kwa mabomba ya maji na walaghai
Mshukiwa mkuu moses simiyu akifichua uwepo wa zaidi ya watu thelathini wanaounganisha maji kiharamu
Kwa sasa kampuni hiyo inaendelea na oparesheni maeneo ya kibomet ,tuwan,nanamgoi kuwanasa wote ambao wanasemekana kushiriki uhalifu huo