WENYEJI WA POKOT MAGHARIBI WASHAURIWA KUMCHAGUA KIONGOZI WA AZIMIO LA UMOJA


Mwenyekiti wa chama cha ODM eneo la Kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Lorien ameendelea kumpigia debe mombea urais wa chama cha muungano wa azimio la umoja one Kenya Raila Odinga akiwataka wakazi wa kaunti hii kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Akizungumza na wanahabari Lorien amemtaja Odinga kuwa kiongozi wa kuaminika ikilinganishwa na wagombea wengine wa kiti cha urais, akielezea Imani kuwa atatekeleza kikamilifu manifesto yake kwa wakenya.
Lorien amesema kuwa maswala mengi ambayo wakenya wanafuriahia kwa sasa ikiwa ni matunda ya ugatuzi yameafikiwa kutokana na juhudi za Raila ambaye alijitolea kuyapigania kwa lengo la kuhakikisha kwamba maisha ya wakenya yanaimarishwa.
Wakati uo huo Lorien ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wagombea nyadhifa za kisiasa kuendesha kampeni za Amani na kutojenga mazingira ambayo huenda yakapelekea migawanyiko miongoni mwa wakazi kwa misingi ya vyama.