WENYEJI WA LESOS TRANS NZOIA WALALAMIKIA UKOSEFU WA MAJI MIEZI MIWILI SASA.


Wenyeji wa Lesos wadi ya bidii viungani mwa mjini Kitale katika kaunti ya Trans nzoia wanalalamikia ukosefu wa maji safi kwa takriban miezi miwili sasa baada ya mwanakandarasi anayekarabati barabra ya Kitale –Suam Kukata mabomba ya maji.
Kwa mujibu wa mwakilishi wadi wa Bidii Peter Waswa hatua ya kurekebishwa kwa mabomba hayo imechukua muda mrefu zaidi huku wenyeji wakihangaika kupata maji safi, shule na vituo vya afya eneo hilo vikikabiliwa na changa moto sawia.
Wakati huo huo Waswa amesema kampuni hiyo ya ujenzi wa barabara imeharibu mabomba ya kusafirisha maji chafu eneo la Vertinary jambo ambalo ni hatari kwa afya ya wenyeji eneo hilo akitoa makataa ya juma moja kurekebishwa kwa mambomba hayo la sivyo aongoze wenyeji kwa maandamano.