WENYEJI WA KIJIJI CHA KOMOL KAUNTI YA POKOT WATAKA HUDUMA ZA MATIBABU KUIMARISHWA


Wito umetolewa kwa Mwakilishi wadi ya Kapenguria na Serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi kuimarisha huduma za matibabu na miundo msingi katika zahanati ya Komol iliyo katika hali mbaya.
Wakiongozwa na wanaharakati Jeff Lomer na Tony Kibet waliozuru kituo hicho Cha afya, wameelezea kusikitishwa na Hali duni ya mazingira , kutokuwepo kwa wauguzi, maji, nguvu za umeme na kutokamilishwa kwa chumba Cha kuwazalisha akina mama.
Kauli ya wawili hao imesisitizwa na wakaazi wa eneo hilo pamoja na David Riongon aliyejitolea kuwahudumia wagonjwa wanaosaka matibabu katika kituo hicho wakimtaka gavana John Lonyangapuo na Mwakilishi wadi Maddy Palokou kuitikia kilio chao.