WENYEJI WA KAUNTI YA TRANSNZOIA WATOA HISIA ZAO KUFUATIA UAMUZI WA MAHAKAMA KUTUPILIA MBALI BBI
Muda mfupi tu baada ya mahakama ya upeo kutoa uamuzi wake kuhusiana na kesi ya mswada wa marekebisho ya katiba kupitia kwa mchakato wa BBI viongozi mbali mbali Kaunti ya Trans Nzoia wamefurahia uamuzi huo wakisema ninafuu kwa wanachi.
Wakiongozwa na mkereketwa wa maswala ya kisiasa katika Kaunti ya Trans Nzoia Philip Matui amesema uamuzi wa mahakama hiyo imedhiirisha uhuru na uwazi wa mahakama hiyo katika utendakazi wake bila ya ushawishi au shininikizo kutoka kwa asasi zingine za serikali.
Matui ambaye pia ametangaza kuwania kiti cha uwakilishi wadi ya sirende eneo bunge la Kiminini kwa chama cha UDA, amesema iwapo mabadiliko hayo ya katiba yangepasishwa mwananchi wa kawaida angelazimika kubebeshwa mzingo zaidi kutokana na kubuniwa kwa afisi na nyadhifa mabli mbali serikalini licha ya gharama ya juu ya maisha nchini kuendelea kupanda, huku wakulima wakipitia wakati ngumu kupata mafuta na pembejeo za kilimo.