WENYEJI WA KACHELIBA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUSAJILI KAMA WAPIGA KURA


Mwenyekiti wa Chama cha ODM katika Eneo bunge la Kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi Samuel Lourien amewarai wakazi wa Kaunti ya Pokot Magharibi kufika katika ofisi za chama hicho ili kujisajili kuwa wanachama.

Akizungumza mjini Kacheliba, Lourien amekisifia Chama hicho akisema kuwa ndicho kinachozielewa changamoto ambazo jamii za wafugaji hupitia.

Lourien ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi wote hasa wakazi wa Kacheliba kujitokeza kwa wingi na kujisajili kuwa wapiga kura katika zoezi la kuwasajili wapiga kura li8naloendelea kote nchini.

Vilevile amewarai viongozi wa Muungano wa OKA kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga katika azma yake ya kuwania urais mwaka ujao.