WENYEJI WA BONDENI KITALALE WAVAMIWA NA FUNZA


Huku msimu wa mvua ukitarajiwa kuendelea, wenyeji wa Bondeni Kitalale kwenye kaunti ya Trans Nzoia wanalalamikia kuhangaishwa na funza.
Kulingana na wenyeji hao ni kwamba hali ya uchochole wanamoishi imekuwa chanzo cha wadudu hao kuwavamia.
Wakizungumzana wanahabari wenyeji hao kadhalika wanasema kuwa ubovu wa nyumba zao pia umechangia wao kuvamiwa na wadudu hao.
Baadhi ya wahisani akiwemu muhubiri Luke Naibei wamejitokeza ili kuzisaidia familia hizo.