WENYEJI WA AKIRIAMET ENEOBUNGE LA SIGOR WAPATA AFUENI BAADA YA KUTENGENEZEWA DARAJA LINALOUNGANISHA KAUNTI YA TURKANA NA POKOT MAGHARIBI.


NA BENSON ASWANI
Ukarabati wa Daraja la Akiriamet eneo Bunge la Sigor litasaidia pakubwa kuleta maendeleo kwa wenyeji ambao wamehangaika kwa muda wanapotaka kusafiri
Akizungumza baada ya kufunguliwa rasmi kwa Daraja hilo Mbunge wa Sigor Peter Lochakapong amesema juhudi za upatikanaji wa amani umerahishwa kwani imekuwa vigumu kukabiliana na wahalifu pindi visa vya uhalifu vinapotokea
Amewataka wakaazi wanaoishi maeneo ya mipakani kudumisha amani hasa msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya
Miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa mashinani inapaswa kutekelezwa na wanakandarasi ambao ni wenyeji
Ndo kauli yake mbunge wa kacheliba Mark Lomnokol ambaye anasema baadhi ya wanakandarasi wamekuwa wakifanya kazi duni na kuwasababishia wananchi hasara licha ya fedha nyingi kutumika
Aidha Lomnokol amemtaka Gavana Longanyapuo kuwekeza rasmali na nguvu zake katika kuwasetiri wananchi na ukame badala ya kujikita zaidi katika maswala ya kisiasa