WENYEJI TRANS NZOIA WAMLAUMU MWANAKANDARASI KWA KUTOZINGATIA MASHARTI NA SHERIA ZOTE ZA BARABARA NCHINI.


Wenyeji kaunti ya Trans-Nzoia wanalalamikia hali mbovu ya magari ya mwanakandarasi wa China State Construction Engineering Corporation anayekarabati barabara kuu ya Kitale -Suam kwa kila ametaja kutozingatia masharti na sheria zote za barabara nchini.
Kwenye kikao na wanahabari wenyeji hao wanasema hali hiyo inahatarisha maisha ya vijana walioajiriwa kuendesha magari hayo mbali na watumizi wengine wa barabara hiyo
Sasa wenyeji hao wamemtaka kamanda wa trafiki kaunti ya Trans-Nzoia kuyanasa magari hayo na kuyafanyia ukaguzi kabla ya kuruhusu kuendelea na kazi yao.
Aidha wenyeji hao wamesema kuendelea kuhudumu kwa magari hayo katika barabara za eneo hilo ni kinyume cha sheria na kutaka mamlaka ya kutathmini sheria za trafiki NTSA kufanya uchunguzi wao na kumchukulia hatua za kisheria mwanakandarasi huyo.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya waziri wa usalama wa ndani ya nchi Dkt Fred Matiang’i kulalamikia utendakazi wa mwanakandarasi huyo.