WENYEJI BUNGOMA WAHANGAKIA KUTAFUTA MATIBABU KUTOKANA NA MGOMO WA WAUGUZI AMBAO UMEINGIA SIKU YA NNE


Wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya Bungoma wamewachwa wakihangaika baada ya usimamizi wa hospitali hiyo kuamuru ifungwe na kuwataka wagonjwa kuondoka mara moja.
Kwenye notisi iliyotolewa na usimamizi wagonjwa wote wametakiwa kuondoka ila tu baada ya kukamilisha malipo.
Kulingana na usimamizi wa hospitali hiyo ya Bungoma ni kwamba hii ni kutokana na ukosefu wa wauguzi na maafisa wa kiliniki wanaoshughulikia wagonjwa kufuatia mgomo wao ambao unaendelea
Baadhi ya wagonjwa waliozungumza na kituo hiki cha Kalya Radio wamesema kwamba hawana pesa za kulipa gharama za matibabu huku wakitoa wito kwa serkali kumaliza mgomo ambao unaendelea.