WENGI WA WASICHANA NA AKINA MAMA KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI WANAKOSA VISODO


Mamia ya wasichana na akina mama katika kaunti ya Pokot Magharibi wanakabiliwa na changamoto za kukosa visodo sababu ya ukosefu wa raslimali hali ambayo inaathiri masomo yao wakati huu wa corona.
Wasichana wengi na akina mama katika katika kaunti hii hawawezi kudhibiti hedhi zao kwa njia salama na heshima na wanakabiliwa na unyanyapaa na aibu kutokana na changamoto hizo.
Akizungumza na kalyaradio Mratibu wa shirika la Pokot Girl Child Network Bi Teresa Lokichu anasema kuwa wasichana wengi wanaendelea kukumbwa na changamoto za kiakili kuambatana na hedhi.
Alisema kuwa wasichana wengi wanawacha shule kutokana na kukosa sodo.
Lokichu alitoa wito kwa viongozi wa eneo hili kuingilia kati na kutatua shida hii ambayo inaathiri wasichana wa eneo hilo.
Kiongozi huyo alisema kuwa kwa sasa,wazazi wengi katika kaunti hii ya Pokot Magharibi hawajaelewa umuhimu wa taulo hizo na pia wengi hawana uwezo wa kuzinunua.