WAZIRI WA ELIMU AENDELEZA UKAGUZI WA UFUNGUZI WA SHULE


Waziri wa elimu profesa George Magoha anaendelea kuzuru shule mbalimbali kutathmini hali ya ufunguzi wa shule shughuli ambayo ilianza hapo jana huku leo akizuru kuanti ya Nyeri. Akizungumza huko Nyeri waziri magoha ameendelea kutetea kauli yake kwamba walimu wanaweza kuwafunza wanafunzi wakiwa chini ya mti na ameelezea kufurahishwa na hali ilivyo katika eneo hilo.
Magoha kwa mara nyingine amekariri kwamba wanafunzi wote walio katika shule zilizoko katika mitaa ya mabanda watapata maski kwa ufadhili wa serikali.
Magoha pia amearifu kwamba wizara ya elimu imetenga shilingi milioni kumi kusaidia shule katika maeneo yanayokumbwa na maafuriko ilikuwapiga jeki katika kukabiliana na changamoto zinazotokana na hali hiyo hususan kaunti ya Kisumu na ile ya Baringo.
vilevile pia ameongeza kwamba fedha zilizotengewa mpango wa kurejea shuleni zilitumwa hapo jana