WAZIRI WA BARABARA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI ATETEA UBOMOZI WA MADUKA MJINI MAKUTANO


Waziri wa bara bara kaunit hii ya Pokot Magharibi Augustine Monges amejitokeza na kukana madai ambayo yamekuwa yakiibuliwa kwamba hakuwa wametoa notisi kwa ubomozi wa maduka ambao ulifanyika wiki hii mjini Makutano kaunit ya Pokot Magharibi.
Kwenye mahojiano ya kipekee ndani ya Mpigo wa Kalya Radio mapema leo, Monges amesema kuwa notisi ilitolewa miezi mitano iliyopita lakini wamiliki wa maduka hayo walipuuza.
Ikumbukwe viongozi mbali mbali kwenye kaunti hii ya Pokot Magharibi waikashifu ubomozi huo wakisema kwamba hawakuwa wamepewa natosi akiwemo Ozil Kasheusheu ambaye ni mwakilishiwadi maalum katika kaunti ya Pokot Magharibi
Naye mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto amesema ubomozi huo haukufuata sheria na kwamba ingelifaa mmiliki wa nyumba hizo kupewa kibali cha mahakamani kwanza akisema ubomozi huo ni gushi.
Mwathiriwa ambaye tumesema naye hata hivyo amesema kwamba serikali ya kaunti hii ya Pokot Magharibi ilikuwa imempa idhini ya kufanya ujenzi kwenye eneo hilo.