WAZIRI MUNYA ATAKIWA KUSHUGHULIKIA MASLAHI YA WAKULIMA WA MIWA MAGHARIBI YA NCHI
Mbunge wa kanduyi kaunti ya Bungoma Wafula Wamunyinyi amemtaka waziri wa kilimo Peter Munya kubuni kamati maalum itakayoshughulikia masaibu ambayo wakulima katika kiwanda cha sukari cha Nzoia wanapitia.
Wamunyinyi amesema kuwa hatua hiyo itahakikisha kuwa wakulima hao wanalipwa kwa wakati, kauli inayojiri baada ya wakulima wa miwa kuandamana wakilalamikia kutolipwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Wakati uo huo Wamunyinyi ameagiza idara husika kufanya ucnhunguzi kuhusu madai ya ufisadi katika kiwanda katika kiwanda cha nzia ili kuepusha uwezekano wa kiwanda hicho kusambaratika.