WAZIRI MAGOHA AZUA MDAHALO BAADA YA KUZUBAA KWENYE STEJI.


Waziri wa Elimu Pro. George Magoha alizua mjadala mtandaoni baada ya kuonekana amezubaa kwenye jukwaa wakati wa hafla ya mashindano ya muziki.
Magoha ni mmoja wageni ambao walioalikwa kuhudhuria tamasha la mashindano ya muziki katika shule ya upili ya wavulana Kisumu lililokamilika ijumaa wiki jana.
Magoha aliandamana na naibu rais Rigathi Gachagua kwenye tamasha hizo ambapo.
Ni wakati wa tamasha hilo ambapo Magoha na Rigathi walialikwa kwenye jukwaa kujiunga na wanafunzi waliokuwa wakipiga densi.
Huku naibu rais akijikakamua kusakata densi hiyo kwa mtindo uliokuwa ukiendeshwa na wanafunzi hao, Magoha alisalia kuzubaa bila kutingika katika kati ya wanafunzi na viongozi wengine waliokuwepo jukwaani.
Si mara ya kwanza kwa waziri huyo kujitia hamnazo wakati viongozi wengine wanasakata densi na kunengua kiuno.
Hapo awali alisalia amesimama wakati mawaziri wengine walijiunga na aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta kunengua kiuno wakati wa ziara yao bado mjini Kisumu.
Hata wakati akicheza naibu rais Rigathi Gachagua alionekana akizungusha mwili wake bila kuandamana na midundo ya wimbo uliokuwa ukichezwa.