WAZEE WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA VITENGO VYA USALAMA KUKABILI UHALIFU KERIO VALLEY.
Mshirikishi wa serikali katika bonde la ufa George Natembeya amewataka wazee kutoka kaunti ya Baringo, Elgeiyo marakwet, na Pokot magharibi kushirikiana na maafisa wa polisi na machifu ili kukabili utovu wa usalama kwenye kaunti hizo.
Akizungumza kwenye kikao na wazee na maafisa wa utawala kutoka kaunti hizo natembeya amesema kuwa suluhu ya utovu wa usalama itapatikana iwapo wazee watakuwa kwenye msitari wa mbele kuhimiza amani baina ya jamii za kaunti hizo tatu.
Natembeya aidha amesema kuwa mashambulizi ya mara kwa mara yanayotokea hasaa katika bonde la kerio huchagiwa na matukio ya ulipizaji wa kisasi.
Wakati uo huo natembeya amesema kuwa usalama utaimarisha uchumi wa maeneo hayo kwani vita vya kila wakati huathiri biashara pakubwa