WAZEE TRANS NZOIA WATAKA CHANJO YA CORONA KUTOLEWA MAENEO YA MASHINANI

Wazee katika kaunti ya Trans nzoia wametoa wito kwa wizara ya afya kuhakikisha kuwa chanjo dhidi ya virusi vya corona inatolewa katika maeneo ya mashinani ili kuepuka umma ambapo huenda wakaambukizwa virusi hivyo.

Ni wito ambao umetolewa na wazee hao kufuatia foleni ambazo zilishuhudiwa katika hospitali ya kitale level 4 wakati walipofika kutoka maeneo bunge mbali mbali ya kaunti ya trans nzoia kupokea chanjo dhidi ya virusi hivyo.

Ni wito unaotolewa wakati mwenyekiti wa kamati ya afya katika bunge la kaunti ya Trans nzoia Daniel Kaburu akiwataka wote ambao wanajitokeza kupokea chanjo hiyo kuwa makini zaidi na kuepuka mikusanyiko ili wa kuzuia kuambukizwa virusi hivyo.

Kaunti hiyo ya Trans nzoia ilipokea chanjo alfu 6000 ya astrazeneca