WAZEE KAUNTI YA UASINGISHU WATOA WITO KWA VIONGOZI KUENEZA AMANI


Baadhi ya wazee wa jamii ya kalenjin katika kaunti ya uasin gishu wameelezea kuunga mkono ripoti ya tume ya uiano na utangamano wa kitaifa ncic inayoiorodhesha kaunti hiyo miongoni mwa sita zinazoweza kushuhudia machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa agosti 9.
Wazee hao ambao wanamuunga mkono mgombea huru wa kiti cha ugavana zedekiah bundotich alias buzeki wamedokeza kwamba kuna viongozi wanaolenga kutatiza azma ya wagombea huru kwenye kaunti hiyo.
Wakizungumza na wanahabari mjini eldoret, wakiongozwa na philip kipkosgei wameweka wazi kuwa baadhi ya viongozi wanawatumia vijana kuzua vurugu na kutatiza kampeni za baadhi ya wawaniaji.
Wazee hao wamewashauri wanasiasa wanaoendeleza mipango ambayo huenda yakazua migawinyiko kusitisha shughuli hizo na badala yake kuwa tayari kupambana na wapinzani wao kwa kutumia sera.
Kwa upande wake mzee philip kipkosgei amependekeza wanasiasa wote wanaowania nyadhifa mbali mbali kuandaa mkutano mmoja wa amani ambao utatumika kuhamasiha umma kuhusu amani.
Kulingana na ripoti ya ncic iliyotolewa juma nne wiki hii ni kwamba kuna uwezekano wa ghasia kushuhudiwa kwenye kaunti za uasin gishu, nairobi, nakuru, kericho, kisumu, na mombasa kabla wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi agosti.