WAZAZI WAUNGA MKONO HATUA YA KUFANYIWA UKAGUZA MTAALA WA UMILISI CBC
Chama cha kitaifa cha Wazazi katika kaunti ya Transnzoia kimeunga mkono mpango wa Rais Wiliam Ruto kuwashirikisha washikadau katika sekta ya Elimu kutathmini upya mtalaa wa umilisi cbc.
Mwenyekiti wa chama hicho Wellington Waliaula amesema wakati umefika kusawazisha Karo na kulainisha Kalenda na sekta ya Elimu kwa jumla
Waliaula amesema ni jambo la kusikitisha kwamba baadhi ya Wakuu wa Shule huitisha karo na ada ya ziada bila ya kuwapa wazazi risiti za kuonyesha kwamba wamelipa huku wanafunzi na wazazi wakiibua maswali na malalamishi wakipuuzwa.