WAZAZI WATAKIWA KUZINGATIA ELIMU YA MTOTO WAKIKE POKOT MAGHARIBI.

Na Benson Aswani
Wazazi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuzingatia umuhimu wa wanao hasa wa kike na kujitenga na hulka ya kuwalazimishia ndoa za mapema na badala yake kuwapa fursa ya kupata elimu.
Akirejelea kisa ambapo wanafunzi watatu kutoka eneo la Pokot kaskazini wamedaiwa kulazimishiwa ndoa za mapema, mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya st. Elizabeth Carolyne Menach amesema tamaduni kama hizo zimepitwa na wakati na ni wakati sasa watoto wa kike wanapasa kupewa fursa ya kupata elimu.
Menach amesema kuwa elimu ya mtoto imelindwa kikatiba huku akitoa wito kwa wadau ikiwemo machifu na wazee wa mitaa hasa eneo la pokot kaskazini kufuatilia swala hili na kuhakikisha kuwa watoto wote wanaopasa kuwa shuleni wanahudhuria masomo.