WAZAZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA WANAO MSIMU HUU WA SHEREHE NYINGI.


Wazazi kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kutumia muda huu ambapo wanafunzi wamefunga shule kwa likizo baada ya kukamilika muhula wa pili kuwa karibu na wanao ili kufuatilia mienendo yao.
Ni wito wake katibu katika wizara ya jinsia, mipango maalum, na huduma za umma Micah Powon ambaye amesema hasa ikizingatiwa huu ni msimu wa sherehe nyingi ipo haja kwa wazazi kuwa makini zaidi ili wanao warejee shuleni muhula ujao wakiwa katika hali nzuri ya kuendelea na masomo.
Wakati uo huo Powon ambaye pia ni mwenyekiti wa shule ya upili ya our lady of peace pser, amewataka wazazi kutumia kipindi hiki kutafuta karo ya wanao kwa ajili ya muhula ujao ili wapate wakati mwema shuleni shule zitakapofunguliwa.