WAZAZI WATAKIWA KUTONYAMAZIA VISA VYA DHULUMA DHIDI YA WATOTO.


Wazazi wametakiwa kuripoti visa vyovyote vya dhuluma dhidi ya watoto wadogo.
Tume ya kitaifa ya usawa wa kijinsia imesema hayo wakati wa kuhamasisha wananchi kuhusu sheria za kukabili dhuluma za kijinsia katika kaunti ya Baringo
Mwenyekiti wa tume hiyo Dr. Joyce Mwikali amesema wasichana wengi walipachikwa mimba mwaka uliopita shule zilipofungwa kutokana na janga la corona.
Amesema haki za wasichana hao ambao wengi ni wenye umri mdogo wa kati ya miaka kumi na miwili na kumi na minane zilikiukwa huku hatua za kisheria zikikosa kuchukuliwa kabisa.